Simba SC leo wamereje kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kufuatia ushindi wao wa magoli 8-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga inayofundishwa na kocha Juma Mgunda, game ilichezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Magoli ya Simba SC yalifungwa na Emmanuel Okwi aliyefunga magoli matatu dakika ya 11, 20 na 47 wakati Meddie Kagere akifunga magoli matatu pia dakika ya 69, 75 na 83 huku Hassan Dilunga na Cloutous Chama wakifunga goli moja moja kila mmoja.
Baada ya game kocha wa Coastal Union ambayo pia inachezewa na staa wa Bongo Fleva Alikiba, kocha wao Juma Mgunda aliongea na waandishi wa habari na kusema wamevuna walichopanda, huku akilalamikia uchovu wa wachezaji wake wa kutoka Tanga na kufikia kucheza leo ndio umechangia.
Simba SC sasa kwa ushindi huo wanarudi kileleni huku wakiwa na viporo vya kutosha kwani wamefikisha point 81 na kuishusha kileleni Yanga iliyokuwa nafasi ya kwanza kwa sababu kwa sasa ina point 80, huku imcheze michezo 34 wakati Simba SC imecheza michezo 31 hivyo ni tofauti ya michezo mitatu, huku Coastal Union ikiwa nafasi ya 10 kwa kuwa na point 41 na imecheza michezo 34.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania