Kuelekea mchezo wa UEFA Champions League kati ya Liverpool dhidi ya Napoli Jumanne usiku wa December 11 2018, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemaliza tetesi za kudaiwa kuwa yuko mbioni kuondoka England na kwenda kufanya kazi Italia.
Liverpool ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 watahitaji kushinda walau goli 1-0, Klopp pia alimtania Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis kuhusiana na madai ya kuhamia Italia.
“Bado nina mkataba wa miaka mitatu na nusu hapa (Liverpool)sina uhakika kama kuna mtu atanihitaji baada ya mkataba huo, Napenda chakula cha kiitaliano lakini sijui kuzungumza lugha yao”>>>Jurgen Klopp
Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha Jurgen Klopp wa Liverpool aliwahi kuhitajika na club ya Napoli ya Italia miaka mitano iliyopita, wakati huo akiwa anaifundisha Club ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe