Club ya KRC Genk ya Ubelgiji usiku wa May 16 2019 imeingia kwenye historia mpya baada ya kuongeza idadi ya mataji yake ya Ligi Kuu Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League, KRC Genk leo walicheza dhidi ya Anderlecht ugenini na kulazimishwa sare ya kufungana magoli 1-1.
Ubingwa wa KRC Genk umekuja kufuatia mpinzani wao mkuu Club Brugge kukubali kufungwa kwa magoli 2-0 dhidi ya Standard de Liege na kufanya Genk kuwa Bingwa wa michuano hiyo wakiwa wamesalia na michezo mmoja mmoja, Genk wana point 51 na Brugge 47 hivyo hata KRC Genk akipoteza mchezo wake wa mwisho na Brugge akishinda hawezi kuzifikia point za Genk.
Baada ya ushindi huo wa nne wa KRC Genk toka walipotwaa kwa mara ya kwanza 1999, 2001 na 2002 sasa wametangaza ratiba yao ya kusherehekea Ubingwa wao kuanzia kesho May 17 2019, Samatta sasa ataingia katika vitabu vya rekodi kama akiendeleea kuwepo KRC Genk msimu wa 2019,/2020 kwani ndio watakuwa wachezaji UEFA Champions League.
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC