Kituo cha matangazo cha Aljazeera leo kimetangazwa kufungiwa kufanya kazi katika nchi ya Sudan kwa muda usiojulikana, bado haijajulikana sababu kamili ya kuwafungia wafanyakazi wa kituo hicho cha kimataifa cha habari kufanya kushughuli zao za kiuandishi,
Taarifa hizo zinakuja ikiwa zimepita siku toka taifa la Sudan limuondoe madarakani aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Omar Al-Bashir na sasa nchi hiyo ikiongozwa na Kiongoz wa Baraza la Mpito la kijeshi la nchi hiyo Abdelfattah Al-Burhan.
Mamuzi hayo yametangazwa baada ya mamlaka husika kudai kuwa kikundi kinachopinga mapinduzi hayo kimekuwa tishio kwa nchi hiyo na kuagiza Aljazeera kuzima mitambo yao iliyopo katika mjii mkuu wa nchi hiyo Khartoum huku kukiwa hakuna sababu zozote.
Imekuwa ni kawaida kwa vituo vikubwa vya habari duniani kuwa na waandishi katika nchi mbalimbali duniani lakini Sudan leo imetangaza kuzuia waandishi wa Aljazeera ambao wamekuwa wakiripoti hali za kisiasa za nchi hiyo kwa ukaribu mkubwa kwa muda mrefu hususani toka Mapinduzi hayo kufanyika.