Baada ya kuangukia kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Everton kwenye ligi wikendi iliyopita, Arsenal wanatarajia kufanya vizuri Alhamisi hii watakapocheza kwenye Europa, ‘The Gunners’ wako nyumbani kukabiliana na Napoli kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya Europa League. Mechi hii ni muhimu sana kwa Arsenal hasa baada ya kupoteza mchezo wa weekend iliypita.
Arsenal kama ilivyo kwa Napoli wanaona Europa sio shindano la kiwango chao hivyo wanatamani kucheza UEFA Champions League, ambayo Arsenal kwa misimu miwili iliyopita wameshindwa kufuzu kushiriki, na msimu huu pia bado wako kwenye hati hati ya kupata timeti ya kufuzu tena kwa kutafuta point ili kumaliza TOP 4 katika Ligi yao.
Baada ya kufungwa na Everton walikuwa mbele ya Chelsea kwa tofauti ya magoli, kila mtu kwenye club anajua kwamba wakishinda Europa basi moja kwa moja watashiriki lUEFA Champions League msimu ujao bila kujali wamemaliza katika nafasi gani kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Napoli wao watacheza michezo yote miwili bila kuwa na presha hiyo kwani wako katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Serie A, kwa upande mwingine Chelsea nao wanagombania vita mbili kama Arsenal.
Wanacheza ugenini dhidi ya Slavia Prague kwenye mchezo wa kwanza ambao wanatarajiwa kushinda, wamekuwa kwenye kiwango kizuri katika shindano hili, wameshida michezo yote 10 na kuunga magoli ya kutosha, huku wakiongozwa na mfaransa Olivier Giroud ambaye amefunga mara tisa msimu huu.
Japokuwa hawapewi nafasi sana, Slavia wameonyesha wana kila uwezo wa kufanya vizuri. Mzunguko uliopita waliwatoa wazoefu wa shindano hilo timu ya Sevilla hivyo Chelsea ni vyema wakawa makini, michezo mingine ni kati ya Benfica na Eintracht Frankfurt, huku Valencia na Villarreal wanakutana katika mchezo wa wahispania pekee, game zitaonesha ST World Football.
Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys