Hii ni nyingine ya kuifahamu kutoka kwa mwanamitindo na mwanamuziki Dillish Mathews kutokea Namibia ambaye wengi tulimfahamu kupitia ushindi wake wa Big Brother Africa lakini amekuwa akihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mchezaji mpira Emamnuel Adebayor anayecheza club ya İstanbul Başakşehir ya Uturuki.
Tetesi za uhusiano wa kimapenzi kati ya Dillish na Adebayor zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii mwisho wa mwaka 2017 baada ya baadhi ya picha kuwaonyesha wawili hao wakiwa pamoja ingawa wamekuwa wakijaribu kufanya mapenzi yao yawe siri.
Penzi kati ya Dillish Mathews na Emmanuel Adebayor linasemekana kuingia doa baada ya comment ya Emmanuel Adabayor katika post ya Dillish kupitia instagram account yake
Dillish aliuliza swali kwa mashabiki zake na kusema “Ni kitu gani cha muhimu ungependa kuifundisha dunia?” Emmanuel Adebayor alionekana kujibu swali lile na kusema “Jinsi ya kuheshimu mawazo ya mtu”
Steve Nyerere “Maisha yamekuwa Magumu lini kwako yamekuwa mepesi”