Rapper Drake kutokea Canada aliziteka headlines za mitandao yote duniani baada ya kutuonesha ndege yake binafsi (Private Jet) kupitia ukurasa wake wa instagram na kupewa jina la ‘Air Drake’ na aliandika caption ‘Hakika hakuna kitu kilichokuwa sawa’.
Inaelezwa kuwa ndege hiyo binafsi imekuja kutokana na dili ambalo Drake alisaini na kampuni ya Cargo Jet, ambapo kampuni hiyo ya ndege ina makazi yake nchini Canada. Inaripotiwa kuwa Mmiliki wa Cargo Jet, Ajay Virmani ameingia makubaliano ya kibiashara na Drake hivyo kutengenezewa ndege hiyo inatajwa kuwa ni moja ya makubaliano ya mkataba wao.
Kwa taarifa yako Drake anaimiliki hii ndege kwa asilimia 100, Kwenye video anasikika akisema “No Rental, no timeshare, no Co-owners” yaani hajakodi wala hakuna umiliki wa mtu zaidi ya mmoja. Wataalamu wanasema ndege za aina hii (Jumbo Jet) zinafikia bei ya $75 milioni hadi $100 milioni sawa na Bilioni 230 za Kitanzania.
VIDEO: Ommy Dimpoz bado anajiuliza “Ni mimi kweli?”, RIP Dr. Mengi