Mwandishi Mika Ndaba kutoka Mahakamani anaripoti kwamba Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media Limited, Maxence Melo na mmiliki mwenza wa kampuni hiyo Mike William leo August 7, 2017 wamefika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kukana maelezo waliyosomewa ya kulizuia Jeshi la Polisi kuuchunguza mtandao huo.
Melo na William wamekana hayo baada ya kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa katika kesi ya kulizuia Jeshi la Polisi kuuchunguza mtandao wao kwa kuchapisha taarifa za uongo.
Katika maelezo hayo, Melo na William wamekubali wasifu wao, ikiwemo majina, umri, kumiliki mtandao wa Jamii Forum na kukamatwa kisha kufikishwa Mahakamani lakini hata hivyo, wamekana kuhusika na tuhuma za kulizuia Jeshi la Polisi kuuchunguza mtandao huo.
Baada ya kusomewa maelezo hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi August 24, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Katika kesi hiyo inadaiwa Melo na William walizuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao huku ikidaiwa kati ya May 10 na December 13, 2016 maeneo ya Mikocheni, Kinondoni, walilizuia Jeshi hilo kufanya uchunguzi baada ya kuchapishwa taarifa za uongo dhidi ya kampuni ya CUSNA Investment na Ocean Link.
ULIPITWA? Manji amkataa Wakili Kibatala kusimamia kesi yake…kisa? Tazama kwenye video hii kila kitu!!!