Tanzania ikiwa kama mwanachama wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani kupitia BRELA iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara inashiriki mafunzo ya hataza kwa Nchi za Africa Nchini Misri kuanzia tarehe 17/11/2019 hadi 21/11/2019.
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO), Nchi ya Misri na Ofisi ya Hataza ya Misri na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Nchi 15 za Africa.
Tanzania imewakilishwa na Suzana Senso Afisa Mwandamizi kutoka kitengo cha Miliki Bunifu-BRELA.
“Mafunzo haya yana manufaa kwa Taifa letu kwenye masuala ya uvumbuzi ili kuweza kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Viwanda, vumbuzi zinahitajika ili kuwa na Bidhaa na huduma zenye ubora na zenye kukidhi mahitaji ya wananchi, ili kuendana na ulimwengu wa sasa wa Technolojia“
BRELA kama Taasisi iliyo na jukumu la kusajili Hataza (Vimbuzi) imeweza kuiwakilisha Tanzania kwenye Mafunzo hayo ili kuweza kuongeza ujuzi wa namna ya kufanyia kazi Maombi yanyotumwa na wavumbuzi hadi wavumbuzi kuweza kumpatia usajili wa vumbuzi zao (Patent search and Examination).