AyoTV na millardayo.com imezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera kuhusu Mto uliopo katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ambao inadaiwa Mtu akinywa maji yake ana uwezekano mkubwa wa kupata Watoto mapacha kwani mpaka sasa katika Kijiji ambacho Mto huo upo, Kaya zisizopungua 28 zina Watoto mapacha ambao wanadaiwa kupatikana kutokana na Wazazi kunywa maji ya Mto huo.
RC Homera amesema ameombwa na Wananchi kupeleka Wataalamu kwenda kuchunguza kama madai hayo yana ukweli wowote Kisayansi na wapo katika hatua za mwisho kuwapeleka Wataalamu hao.
“Hata mimi mwenyewe nina mpango wa kuyanywa maji hayo ili nione kama naweza kuongeza mapacha angalau wawili”– RC Homera