Ushawahi kujiuliza nani atakuandaaa siku yako ya mwisho pale mwili utakapotengana na roho, nani atakuosha, nani atakuvisha? au ushajiuliza inakuwaje pale mtu anapofariki katika ajali viungo vyake vya mwili vikatengana, utumbo ukatoka nje?.
Maswali hayo yakanifanya nifunge safari mpaka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika chumba cha kuhifadhia maiti wenyewe wanapaita wodi namba 26, hapa miili hutengenezwa kama gari lililopondeka likipelekwa gereji.
Mwili hupigwa msasa kwa kurudishia viungo mahali pake, kazi ambayo hufanywa na wataalamu waliosomea.
Rajabu Shekimweri, mtaalamu wa mochwari ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye amekuwa akifanya majukumu na kuichukulia kazi yake hiyo kama nyingine kwa kipindi cha miaka saba sasa.