Band ya Yamoto tayari imeondoka jana usiku kuelekea Marekani tayari kwa ziara yao ya wiki tatu baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Watanzania wanaoishi huko.
Mkubwa Fella amezungumzia safari hiyo kuwa ni mwaliko walioupata kutoka kwa Watanzania wenzao wanaoishi USA ambapo watakwenda kufanya show na wameondoka na timu nzima ya watu nane.
Akizungumzia show watakazofanya huko Mkubwa Fella amesema..“Itakuwa ni ziara ya wiki tatu na watarejea Tanzania tarehe 16, show ya kwanza watafanya Tarehe 27 Kenshaz City, na ya pili watafanya tarehe 12 huko Washington , hii ni mara ya kwanza kwa Yamoto kupata mualiko kwenda US, nimefurahi sana na kila siku nasema tutaendelea kutoa furaha mpya Marekani, mashabiki wetu wategemee mazuri zaidi“..Mkubwa Fella.
Ameongeza kuwa baada ya ngoma ya ‘Cheza kwa Madoido’ wametengeneza ngoma nyingine inaitwa ‘Mama’ na wanatarajia wakirudi wataachia ngoma yao ambayo wamemshirikisha Zena Mohamed kutoka kundi la Five Stars.
Hapa kuna sauti ya Mkurugenzi wa ‘Yamoto Band’ Said Fella pamoja na kundi la Yamoto wakizungumzia safari yao…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE