Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea hii leo kwa mchezo mmoja uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ukiwakutanisha wenyeji Yanga na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.
Katika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa goli 2-0 katika mchezo ambao walionekana kuutawala kuanzia mwanzo hadi mwisho kitu ambacho kiliwapa nafasi kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi kwa idadi kubwa ya mabao.
Yanga walifunga mabao yote mawili kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alifunga mabao mawili baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa Liberia, Kper Sherman.
Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Coastal Union kwa bao moja.
Matokeo haya yanawafanya Yanga wapande kwenye kilele cha ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na idadi ya pointi 25 wakiwazidi mabingwa watetezi Azam FC kwa pointi tatu.
Nitaendelea kukusogezea kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook