Yanga na Azam FC zimekutana July 29 katika mchezo wa robo fainali ya nne ya Kombe la KAGAME 2015, Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu kwa mujibu wa sheria ya CECAFA mechi za robo fainali na nusu fainali huwa hakuna dakika thelathini za nyongeza hivyo ikalazimika kupigiana penati.
Mchezo umemalizika kwa klabu ya Azam FC kushinda kwa jumla ya penati 5-3 mikwaju ya penati ya Azam FC ilipigwa na Kipre Tchetche, John Bocco, Himid Mao, Pascal Wawa na Aggrey Moris huku penati za Yanga zikipigwa na Salum Telela, Nadir Canavaro, Geofrey Mwashiuya na Haji Mwinyi penati yake kudakwa na Manula.
Kwa matokeo hayo Azam FC itacheza mchezo wa nusu fainali July 31 siku ya Ijumaa
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.