Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Yanga SC Vs Ndanda FC imemalizika. Matokeo na Pichaz nimekusogezea hapa…

on

yanga
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea hii leo kwa michezo miwili iliyopigwa jijini Dar es Salaam pamoja na huko mkoani Pwani ambako timu nne zilikuwa viwanjani zikisaka pointi tatu muhimu.
Jijini Dar es Salaam uwnaja wa taifa ulishuhudia mchezo kati ya mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Dar es Salaam Young Africans dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Ndanda FC toka Mtwara.

Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria mchezo huo kumalizika hakukuwa na timu iliyoweza kumtambia mwenzie baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya bila kufungana.

Hata hivyo Yanga watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na ushindi baada ya kutengeneza nafasi kadhaa za wazi ambazo kama washambuliaji wake wangekuwa makini basi Yanga ingeweza kushinda.

Mshambuliaji raia wa Liberia Kper Sherman alikosa bao la wazi .

Mshambuliaji raia wa Liberia, Kper Sherman alikosa bao la wazi.

Katika mchezo mwingine uliopigwa huko mkoani Pwani kwenye uwanja wa Mabatini wenyeji Ruvu Shooting waliwafunga Stand United kwa mabao mawili kwa moja.

Ruvu Shooting walifunga mabao yao kupitia kwa Juma Mpakala kwenye dakika ya tano ya mchezo huku bao la ushindi likija kupitia kwa Yahya Tumbo kwenye dakika ya 89 na Stand United wakafunga kupitia kwa Hamis Thabit.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

Picha zote ni kutoka kwenye screen ya Azam TV.

Matokeo ya michezo ya leo yanawafanya Yanga washindwe kuwafikia Azam FC kwenye kilele cha msimamo wa ligi ya Tanzania Bara ambapo hadi sasa wana pointi 19 wakiwa wamezidiwa kwa pointi mbili na Azam wenye pointi 21.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter,  Instagram  na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments