Saa chache baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera amefutwa kazi, AyoTV ilimfuata Zahera nyumbani kwake na kutaka ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo kuwa amepokea barua au taarifa rasmi.
“Hata kama walifanya mkutano na waandishi wa habari mimi sijapata barua kufukuzwa kazi sasa mimi nitawaita na nitafanya mkutano na waandishi, hakuna dalili hata iliyokuwa inaonesha kuwa hili litatokea kwa sababu mwenyekiti (DR Msolla) tulivyokuwa Misri tuliongea mengi akasema hata tukipigwa kule Misri hatuwezi kukufukuza”>>>Zahera
Ndani ya msimu wa 2018/2019 Zahera ameiongoza Yanga kucheza jumla ya michezo 10 na kushinda mitatu, kufungwa 4 na sare michezo mitatu, mkataba wa Zahera na Yanga ulikuwa unamalizika September 2020.
VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete