AyoTV

VIDEO: Kocha wa Simba SC kathibitisha, John Bocco inabidi apelekwe Afrika Kusini

on

Kocha Mkuu wa Simba SC ameweka wazi leo wakiwa mazoezini Gymkhana kujiandaa na mchezo wa Alhamisi ya November 7 2019 uwanja wa Uhuru dhidi ya Tanzania Prisons, kuwa mshambuliaji wake John Bocco licha ya kupatiwa matibabu kwa miezi miwili na kufanya mazoezi mepesi lakini bado anasikia maumivu na sasa ataenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

“Unajua Bocco tatizo lake amekuwa akisumbuliwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa na amekuwa majeruhi, bado anasikia maumivu hiyo sio habari njema ila tutampeleka Afrika Kusini akaangaliwe tena na anahitaji kupata ushauri tena kwa mtaalum”>>> Patrick Aussems

Simba SC sasa kwa mujibu wa kocha Patrick Aussems ni kuwa imekuwa na mshambuliaji mmoja pekee Meddie Kagere ndio mzima wakati washambuliaji wake wawili Wilker Da Silva na Miraj Athuman wanaungana na John Bocco katika list ya majeruhi.

VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”

Soma na hizi

Tupia Comments