July 11 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF limetoa taarifa iliyoipata kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF, TFF wametangaza maamuzi ya CAF yalioamuriwa juu ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupigwa faini ya dola 5000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 9.
CAF wamefikia maamuzi hayo kwa kosa la wachezaji wa Yanga kumzonga muamuzi na kuchelewa muda wakati wa mchezo wao marudiano wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya GD Esperanca ya Angola, mchezo ambao ulichezwa May 18 2016 Angola.
Maamuzi hayo yalifanywa na Kamati ya Nidhamu ya CAF inayoundwa Mwenyekiti Raymond Hack – raia wa Afrika Kusini na wajumbe Mustapha Samugabo (Burundi) na Gbenga Elegbeleye (Nigeria), pamoja na Amina Kassem kutoka Sekretarieti ya CAF ambaye ni Mtawala katika Kitengo cha Nidhamu.
IMETOLEWA NA TFF
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1