Matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Yanga 2016 uliofanyika jana June 11 2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam yametangazwa leo June 12 2016, uchaguzi huo ambao matokeo ya awali Yusuph Manji ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti na makamu wake Clement Sanga walionekana kuongoza.
#YusuphManji na makamu wake #ClementSanga wamechaguliwa kwa awamu nyingine tena kuendelea kuwa viongozi wa #Yanga pic.twitter.com/YhutnSIFts
— millard ayo (@millardayo) June 12, 2016
Kwa pamoja Manji na Sanga wamechaguliwa kuiongoza Yanga kwa awamu nyingine tena, Yusuph Manji kashinda kwa jumla ya kura za ndio 1468, hapana 0 na kura zilizoharibika zilikuwa 2, kwa upande wa Sanga ameshinda kwa jumla ya kura 1428 kati ya kura 1508 zilizopigwa huku mpinzani wake Titus Ossoro akipata kura 80 pekee.
Matokeo ya nafasi ya ujumbe #UchaguziMkuu, wajumbe 8 kati ya 20 ndio wameshinda nafasi hizo. 12 #S.Haule (197) pic.twitter.com/e1rORwox0u
— millard ayo (@millardayo) June 12, 2016
KAMA ULIIKOSA MANJI ALIPOFUNGA KAMPENI ZAKE NA KUELEZA KUHUSU UJENZI WA UWANJA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE