April 08 kupitia You heard Soudy Brown aliamplify taarifa za Dudubaya kumkata sikio mama yake mkubwa ikielezwa kuwa anamhisi mama yake huyo anamloga kimuziki ambapo baada ya hizo stori kusambaa, Dudubaya kapatikana na kukubali kuiongelea hii ishu.
Anasema >> ‘hizo taarifa mwenyewe nimekuja kuwasha simu saa 9 kwa sababu ya kukesha juzi, naambiwa bwana unatafutwa hivi na hivi na hizo taarifa mimi mwenyewe nimezisikia kwenye mitandao’
‘Nimepokea pia simu kutoka nchi mbalimbali washkaji zangu wanavyoniambia mimi nipo Shinyanga kwenye biashara zangu, siwezi kuishi kwa kujificha kama digidigi mimi ninafahamika halafu cha kushangaza kama Polisi Mwanza karibu Polisi wote wana namba zangu na hakuna hata mmoja aliyenipigia’
‘Mimi nikiwa na kesi Polisi huwa napigiwa simu bwana eeh kuna tukio hili na hili tunakutafuta na ninaenda mwenyewe, sasa nashangaa sijapigiwa simu na sijui kama kuna kesi kituo gani wala nini, nina wasiwasi hii inshu na ndugu zangu binafsi’
‘Mimi ndugu zangu nawajua vizuri hawa wa ukoo wangu na nilikua siwajui zamani wakati muziki wangu uko juu, kwenye muziki mwaka 2000 nilikua nawajali, nikienda mkoa nawapa kipaumbele cha juu kabisa lakini nilivyokuwa naenda Mwanza kipindi cha nyuma ndugu zangu walikua wanaongea maneno kibao Ooh Dudubaya hajajenga kwao Kisesa hajafanya hivi’
‘Mwisho wa siku nilisikitika nilivyoenda kujenga nyumba kwa ajili ya mama yangu mzazi self container ya vyumba vinne lakini ndugu wakanuna, hakuna anayenipigia simu kuniambia labda hongera wakati kabla walikua wanaongea maneno mengi’
‘Wakatumwa watu kwenda kupiga picha pale nyumbani wakapeleka kwenye gazeti la Sani Watanzania walishawahi kuona hilo gazeti liliandikwa Dudubaya amtelekeza Mama yake mzazi, nilipomuuliza yule Mwandishi akanambia mimi sijafika hata kwenu kuja kupiga picha waliofanya hivyo ni ndugu zako na jamaa zako’
‘Nawajua hao ndugu hata kwenye hili suala wanajaribu kutengeneza vitu fulani kuwa huyu kafanya hivi kumkata sikio mama yake mkubwa kama kunichafulia nionekane namna gani lakini kama kuna kesi Polisi na kama mama yangu huyo mkubwa kasema twende Mahakamani tutakwenda, ninachoamini yule ni mama yangu na mimi ni mwanae’
104.4 Clouds Fm inasikika ukiwa Dodoma.
Bonyeza play kusikiliza.