Wakili anayemtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema,Sheck Mfinanga amejitoa kuendelea kumtetea mteja wake kwa kile alichodai kuomba nakala za mwenendo wa kesi hiyo zaidi ya mara tatu ili akate rufaa mahakama kuu lakini Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru ,Desderi Kamugisha amegoma kutoa.
Mara baada ya wakili huo kujitoa, Mbunge Lema alilazimika kusimama mwenyewe na kasha kumuomba Hakimu Kamugisha kuisogeza kesi hiyo mbele zaidi ili atafute wakili mwingine na endapo akishindwa kumpata atajitetea yeye mwenyewe.
Walipoulizwa mawakili wa serikali Khalili Nuda na Alice Mteng walisema ni haki ya mshtakiwa kupewa muda zaidi ili atafute wakili mwingine hivyo Hakimu Kamugisha akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14 mwaka huu.
Ulipitwa na hii? Wamiliki IPTL/ESCROW wamefikishwa tena Kisutu leo, Maamuzi ya Mahakama je?