Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa familia ya Marehemu Aretha Franklin imeiomba Mahakama ruhusa ya kuuza baadhi ya mali zake alizoacha pamoja na ardhi ili kulipa deni la kodi alilokuwa akidaiwa.
Inaelezwa kuwa Marehemu Aretha Franklin alikuwa akidaiwa na mamlaka ya mapato nchini Marekani kodi ya kiasi cha dola million 6.3 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 14 za Kitanzania, familia ya Aretha imeeleza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kulipa deni hilo aliloliacha ndugu yao ambaye alifariki August 16,2018.
Aretha Franklin alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu na enzi za uhai wake alitambulika kama ”Malkia wa Soul”.
VIDEO: MSHINDI WA MISS MBEYA AKABIDHIWA ZAWADI YA PIKIPIKI ‘BODABODA’