Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Ijumaa ya December 22 2017 ilikuwa katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi kucheza mchezo wake wa round ya pili wa Kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Green Warriors.
Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo, wamekutana na bahati mbaya baada ya kuvuliwa Ubingwa wa michuano hiyo kwa kufungwa kwa mikwaju ya penati 3-4, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika game 1-1, goli la Simba likifungwa na John Bocco kwa penati dakika ya 54.
Baada ya kufungwa afisa habari wa Simba Haji Manara aliandika hivi instagram “Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaid ya twenty millions… nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..AIBU YA MWAKA”>>>Haji Manara
Mstaafu Kikwete na Zitto Kabwe baada ya Zanzibar kuingia fainali