Leo February 14,2018 ni siku ambayo inafahamika kama siku ya wapendanao (Valentine Day) na hivyo wengi husheherekea siku hii wakiwa na wapenzi wao na hupokea zawadi tofauti tofauti kama maua n.k.
Ila kwa upande wa mzazi mwenzake Diamond Platnumz ambaye ni Zari the bosslady ambaye wengi walitegemea kuwa huenda Diamond Platnumz atakua na mzazi mwenzake huko Afrika Kusini lakini imekuwa ndivyo sivyo.
Kupitia snapchat account ya Zari amepost maneno haya “Happy Valentine’s ni siku ya kawaida kwangu, kwenye kusaka pesa”
Maneno haya ya Zari kupitia snapchat yake yametafsirika kuwa huenda Diamond Platnumz na Zari hawako sawa mpaka sasa kutokana na tetesi zinazoendelea kuhusu Wema Sepetu kuwa karibu na Diamond Platnumz.
Kabla ya mwaka kuisha tarajia Diva The Bawse kuanza kuitwa mama