Rapper Tekashi 69 kutokea Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 4 ikiwa kifungo hicho atakitumikia nje akiwa chini ya uangalizi wa Mahakama hii ni kutokana na kosa la kumtumia kingono msichana wa miaka 13 mwaka 2015.
Kwa mujibu wa upande wa waendesha mashtaka walipanga rapper huyo ahukumiwe miaka 3 jela ambapo Ijumaa ya October 26,2018 Tekashi 69 alipanda kizimbani na kupokea hukumu ya kifungo cha nje cha miaka 4 pamoja na kupewa masaa 1,000 ya kujihusisha na kazi za kijamii.
Kutokana na Tekashi 69 kukiri kosa lake Mahakama imemuamuru kutojihusisha na vikundi vya kihalifu ikiwemo kuepuka kosa lenye uhusiano na matendo ya ngono na kutopost picha au chochote kinachohusu masuala ya ngono kwa watoto na wanawake mtandaoni.
Chege aongelea Collabo yake na Patoranking, aahidi makubwa leo