Kumekuwa na maneno mengi kuhusiana na baadhi ya zawadi zilizotolewa kwa Miss Tanzania 2018 hususani gari alilokabidhiwa usiku wa September 8,2018 huku wengi wakidai kuwa gari hakustahili kupata aina ya gari la Terios.
Muigizaji Steve Nyerere amemtetea muandaji na mtayarishaji wa mashindano hayo Basila Mwanukuzi na kusema kuwa anastahili tuzo ya Malkia wa nguvu kutokana na kile alichokifanya kwa kujitoa ili kukamilisha mashindano ya Miss Tanzania 2018.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Steve Nyerere ameandika“Kama @xxl_cloudsfmtz@cloudsfmtz mtaandaa tena malkia wa NGUVU ,Basi naomba zawadi ya kwanza apewe @basillamwanukuzi ,Ni mwanamke wa NGUVU amejaribu ameweza”
“Lakini kikubwa zaidi nimependa kuna DADA zetu wanaenda kupata ajira kupitia wewe,Kikubwa zaidi uliingiza mikono yako mfukoni na kutoa pesa yako .Kila BINADAMU ana madhaifu yake ,Basi madhaifu yake tunaweka kando .Tunasonga na mazuri yake”
Nay wa Mitego kahoji kazi za wakuu wa wilaya