Penzi kati ya muigizaji Irene Uwoya na staa wa muziki wa Bongofleva Dogo Janja linaonekana kuzidi kupamba moto baada ya wawili hao kuamua kuweka mapenzi yao hadharani na kutokujaliwa wanaowakosoa kwa kupishana kwao umri.
Irene Uwoya azidi kuonyesha mapenzi kwa mume wake Dogo Janja baada ya kuamua kuchora tattoo katika mwili wake nakuandika Abdul ambalo ni jina halisi la mume wake Dogo Janja.
Kupitia instagram account ya Dogo Janja amelithibitisha hilo kwa kupost picha ya bega la Irene Uwoya mahali ambapo ndio amechora tattoo yenye jina la Abdul,
Dogo Janja ameandika>>>“Ahsante Mke Wangu❤️ Nichore Nakule Ninapopaonaga mimi tu🤦🏻♂️👌🏻 @ireneuwoya8 Love U❤️ #MyNameOnHerShoulder #MrsAbdul ☺️”
Irene Uwoya sio staa wa kwanza kwa mwaka 2018 kuonesha hadharani kuwa amechora tattoo yenye jina la mume wake katika mwili wake, kwani Shilole nae siku kadhaa nyuma aliweka hadharani kuwa amechora tattoo yen jina la mume wake ‘Uchebe’
ALL GOALS: Yanga vs Singida United Aprill 11, Full Time 1-1