Siku ya February 14,2018 staa wa muziki nchini Juma Jux aliwasili Burundi kwa ajili ya kufanya show ikiwa ndio mara yake ya kwanza nchini humo ambapo alipokelewa kwa shangwe na baadhi ya mashabiki.
Kupitia instagram akaunti ya Jux ameonyesha kufurahishwa na mashabiki walijitokeza kum-support kwa kuhudhuria show ambayo aliifanya nchini humo na wakati akiwa kwenye stage waliimba pia wimbo wa Taifa wa nchi hiyo.
“Asanteni sana burundi sitaweza kuja kusahau upendo wenu kwenye Maisha yangu japo Mvua kubwa kunyesha bado mkakubali mnyeshewe nakuja kwa wingi sana kwenye show.”
“We made a history nashukuru kwa heshima yenu ya kuniimbia wimbo wa taifa 🙌🏾🙌🏾 kama heshima yenu kwangu na hii haijawahi kutokea kwa Msanii yoyote yani yote aliyeshawahi kuja burundi Asanteni sana sana #love #burundi #history#music #power #africanboyworldwide”
Ukiacha nchi za jirani kama Kenya, Uganda, Burundi ndio taifa lingine la jirani na Tanzania linalocheza nyimbo za Bongofleva Redioni na kwenye Tv
Ulipitwa na maneno ya ZARI “Utakoma tu mwenzangu?”