Kamishna wa Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam Simon Sirro ameeleza kuwa Jeshi hilo bado lipo kwenye upelelezi kuhusu kuvamiwa kwa Clouds Media Group na pindi upelelezi utakapokamilika hatua zinazotakiwa zitafuata ikiwa ni pamoja na kulifikisha jalada kwa Wakili wa Serikali.
Kamanda Sirro amesema hayo mbele ya wanahabari ambao walihoji hatua ambayo upelelezi huo ulipofikia na namna jambo hilo linavyoshughulikiwa: “Kesi ni ushahidi Kwa hiyo ndugu zetu bado tunapeleleza lakini niwaombe ndugu zetu wa Clouds waendelee kutupa ushirikiano, watupe ushahidi…mimi kazi yangu ni kupeleleza…nikishapeleleza ushahidi uliopo napeleka kwa Wakili wa Serikali.” – Kamanda Sirro.
Aidha, mbali na suala hilo Kamanda Sirro alielezea pia kuhusu hali ya usalama wa Dar es Salaam akigusia pia tukio la kuuawa kwa majambazi na kukamatwa silaha moja huku pia akizungumzia kuhusu ukaguzi wa mabasi shule ‘School Bus’.
Kauli ya Waziri Mwigulu kuhusu mauaji ya wenyeviti Kibiti…