Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) imeokoa Shilingi la Kitanzania Milioni themanini na tisa laki saba elfu sabini na tisa na mia tano (89,779,500) kupitia kodi za wapangaji wa Nyumba zinazomilikiwa na Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC)
Akitoa taarifa hiyo mbele ya vyombo vya habari Afisa uhusiano wa ZAECA Yussuf Juma Suleiman amesema hadi kufikia Januari 2021 ZAECA imebaini zaidi ya shilingi bilioni Moja Milioni Mia Tisa Hamsini Laki Nne Sabini na Saba Elfu Mia Tano Kumi na Saba (1,950,477,517/) za Kitanzania ambazo ni deni wanaodaiwa baadhi ya wapangaji wanaoishi katika Nyumba zilizopo zaidi ya maeneo 19 Unguja zinazomilikiwa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC)
Yussuf Amesema hadi kufikia Febuari 22 Mwaka huu ZAECA imeokoa Kodi za shilingi Milioni Themanini na Nane laki Saba Sabini na Tisa na Mia Tano (88,779,500) za Kitanzania kutoka kwa wapangaji hao
Aidha amesema zoezi hilo linaendelea na kuhakikisha Fedha zote zinalipwa hivyo amewataka wananchi waliopangishwa katika nyumba hizo kuhakikisha wanalipa madeni yao ili kuepuka usumbufu.