Zaidi ya madereva na matingo 1,200 wa Tanzania pamoja na malori 600 yanayomilikiwa na wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania wamekwama nchini Zambia baada ya kuzuiliwa nchni humo.
Maroli hayo ambayo yanasafirisha mizigo (magogo) kutoka nchini Congo DR na Zimbambwe yamezuiliwa nchini Zambia kwa zaidi ya siku 60 sasa jambo ambalo husababisha hasara kwa wamiliki wake ambao hupoteza zaidi ya dollar 6 million kwa kuingia gharama kuwahudumia watu hao.
Ayo TV na millardayo.com imezungumza na Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania TATOA ili kujua hatma ya madereva, matingo na malori ambapo wameelezea hasara wanayoipata kwa malori hayo kuzuiliwa ambao licha ya hasara hizo pia usalama wa watanzania hao ni mdogo katika eneo walipozuiliwa.
Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi inafuatilia zaidi kuhusu suala hilo ili kumaliza mzozo uliopo na watanzania waliokwama huko warejeshwe nchini ikiahidi kulipatia ufumbuzi suala hilo hadi April 25, 2017.
Bonyeza play hapa chini kutazama…
VIDEO: Kimetajwa kiwango cha mbegu za maharage kinachohitajika na wakulima Tanzania. Bonyeza play kutazama.