Zari ambae ni miongoni mwa waliojifungia majumbani nchini South Africa ili kujikinga na corona amepaza sauti kuhamasisha Watu watulie majumbani kama hawana mizunguko inayowalazimu kutoka, hii yote ni kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Kwenye live na followers wake Instagram Zari amesema anaamini kutulia na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima kutasaidia, anasema amekua akitoka mara chache kufata chakula na vitu vingine kwenye super market na kila anaporudi nyumbani hulazimika kupuliza dawa vya kutosha ili kujikinga.
Bonyeza hapa kumtazama Zari akiongea kuhusu corona HAPA
Mpaka sasa Nchi ya South Africa ina Wagonjwa wa corona 1655 huku vifo vikiwa 11 ambapo Taifa hilo bado linapambana ili waweze kuwa na uwezo wa kupima Watu 30000 kwa siku.
MGONJWA WA CORONA ALIHISI AMEWEKEWA SUMU, AMEPATIKANA ZANZIBAR AMETOKEA TANGA
ZARI KUHUSU TANASHA, AJIANDAE KUMLEA MTOTO WAKE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA