Inawezekana kabisa kuna watu wangu wengitu wanavipaji vyao ikiwemo vya kuimba na bado hawajajua ni lini watapata walau fursa ya kujitokeza kuvionyesha na baadae kuvitumia kama sehemu ya kujipatia kipato cha maisha yake, yes good news kutoka katika kampuni ya HIGH TIME MARKETING AND PROMOTION CO LTD imeliona hilo na kuamua kutoa nafasi kwa watu wake wa Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa shindano hilo Masudi Kandoro amesema…’High time tumeona kuna haja ya kujenga mfumo wa uzalishaji vipaji vya waimbaji wa singeli kwa kutoa fursa kwa vijana ambao tunaamini watakuwa chachu ya kuutangaza muziki wa Tanzania‘
‘Katika mashindano hayo tunatafuta mshindi mmoja ambaye atapata zawadi yenye thamani ya shilingi milioni 10 ambayo itagawanywa ifuatavyo;-
. Pesa taslimu
. Kusimamiwa mizuki wake chini ya High Time
. Kurekodi album yake ya audio
. Kufanyiwa video tatu zenye viwango vya kimataifa
. Kutangaza muziki wake ndani na nje ya nchi
ULIIKOSA ILIVYOKUWA KWENYE MAPOKEZI YA RAIS MAGUFULI MWANZA