Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Septemba 20 ,2021 ameshiriki mkutano wa umoja wa Mataifa uliojadili kuhusu athari za Mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoikumba dunia na kusisitiza umuhimu wa kutopuuzia juhudi za kukabiliana na janga hilo.
“Tuko katika kipindi ambacho wakati tunapambana na athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchini bado tunataabika na chanamoto kubwa ya sasa ambayo ni Ugonjwa wa Virusi vya Korona, Uviko-19 ambasyo imeangusha sana hali ya Uchumi na kufuta mafanikio yaliyokwisha katika miongozi kadhaa ya kujenga jamii zetu”- Rais Samia
Mhe Rais Samia amesisitiza pia kuwa ingawa watu wengi wanachukulia kirahisi kupanda kwa hali ya joto kama moja ya athari za mabadiliko ya Tabia nchi, bado hali ni kusikitisha kwa nchi kama Tanzania kwani hali hiyo husababisha ukame ambao ni athari mbaya kwa sekta zinazotegemea maliasili kama vile kilimo, uvuvi, na misitu ambazo zinachangia 30% ya pato la Taifa na kuathiri takribani 60% ya Wananchi.
TAZAMA MSAFARA WA RAIS SAMIA NCHINI MAREKANI, AWASILI NEW YORK