Leo Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga alitembelea ofisi za zimamoto na kujionea changamoto mbalimbali zinazolikabili jeshi la uokoaji.
Uhaba wa vifaa..”Kuna haja ya kutafuta maeneo mengine ya kuweka vifaa, hali ya eneo ya kuhifadhia vifaa halijabadilika, Ni kweli bajeti ni ndogo lakini nimeongea na uongozi kuhakikisha wanakusanya mapato ili kupata vifaa vya kutosha“..
Adhabu kwa madereva wasioheshimu magari ya zimamoto...”Sasa hivi tunajenga barabara za mabasi yaendayo kasi, tutarahisisha wenzetu wa zimamoto waweze kupita sehemu hiyohiyo ili waweze kufika haraka kwenye tukio..Madereva wawe wepesi wa kupisha magari yanayokwenda kwenye dharura, yawe ya wagonjwa ama yale ya zima moto na wale wanaokiuka wachukuliwe sheria kali…Kitwanga
Mipango ya kupata vifaa vya kisasa…“Katika viwanja vya ndege tuna magari ya zimamoto ya kisasa sana, tuhakikishe tunajipanga vizuri kuhakikisha tunapata vifaa imara na vya kisasa zaidi“..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.