Premier Bet
TMDA Ad

Mix

VIDEO inayoonyesha Rais Mugabe akianguka kwenye ngazi

on

Mugabe

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe tumesikia mara nyingi akiwa na migogoro na mataifa ya Ulaya, Marekani ishu kubwa ni kitendo cha Mugabe kuonekana akiendelea kung’ang’ania madaraka kwa kipindi kirefu.

Video, picha na story kubwa mitandaoni kwa sasa ni ishu ya Rais huyo kuanguka wakati akishuka ngazi baada ya kuhutubia wanachama wake Harare, baada ya kumaliza kuhutubia alisalimiana na viongozi kadhaa wa Chama hicho halafu akawa anashuka ngazi, akaishiwa nguvu na kuanguka chini, walinzi wakamuinua na kumpeleka kwenye gari yake.

Mugabe-7

Kwenye video Mugabe anaonekana akishuka ngazi lakini hali yake ni kama mgonjwa au mtu aliechoka.

https://www.youtube.com/watch?v=txiJ9i375Gc

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments