Una haki ya kupata chochote kinachonifikia mtu wangu wa nguvu hii baada ya kuipata nimeona haitokua nzuri kama nisiposhirikiana na wewe kuisoma hii kuhusiana na maneno ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini , Mh Zitto Kabwe kutaja kiasi cha fedha ambacho kitahudumia deni la taifa katika bajeti ya 2016/17.
Mbunge huyo alishea taarifa hiyo kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook na kusema..>>>’Shiling trilioni 8 kuhudumia Deni la Taifa katika Bajeti ya 2016/17, nimemaliza kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu. Kimsingi ni Bajeti ya kulipa Deni la Taifa’– Zitto Kabwe
‘Wakati Serikali inatarajia kukusanya tshs 17 trilioni mwaka huu, tshs 8 trilioni takribani 50% italipia Deni la Taifa. Ukiweka na Mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya Bajeti, ina maana makusanyo yote ya Serikali yatalipia madeni na mishahara. Ndio maana Serikali inaenda kukopa zaidi tshs 7trn mwaka huu na kutegemea misaada ya wafadhili kwa tshs 5 trilioni’ – Zitto Kabwe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUABE
KAMA ULIKOSA HII RIPOTI YA TUHUMA ZA RUSHWA, WAZIRI MKUU KAZUNGUMZA HAPA ITAZAME HAPA