Mbunge wa Kigoma ambaye ni Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amewasili Mahakamani pamoja na Mawakili wake, kusubiri hukumu dhidi ya kesi yake ya uchochezi huku akiwa tayari amesha nyoa kipara.
Hukumu hiyo ya kesi ya uchochezi, inayotarajiwa kuvuta hisia za watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania, itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Kesi hiyo iliyofunguliwa tarehe 2 Novemba 2018 na Jamhuri, itahitimishwa leo kwa Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, ama kutupwa gerezani, kupigwa faini, au kuachiwa huru.
Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Chama cha ACT –Wazalendo, alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.
WATU 87 WANAODIWA KUUA WAKAMATWA MBEYA