Leo May 29, 2020 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Kiongozi wa Chama cha Wazalendo, Zitto Kabwe kutotoa wala kuandika maneno ya uchochezi kwa muda wa mwaka mmoja.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, baada ya kumtia hatiani Zitto Kabwe katika mashitaka matatu yaliyokuwa yakimkabili mahakamani hapo.
Hakimu Shaidi amesema kuwa maneno aliyoyatoa Zitto hayana ukweli, makali na magumu mno ambayo yameshindwa kuthibitishwa kwenye utetezi.
Ni Maneno ambayo hayana ushahidi wa kutosha, hakuna palipothibitishwa kwamba askari wamemua nani na ushahidi unaonesha tukio lilifanyika alfajiri muda ambao huwezi kusema nani alimua nani ”
“Maneno yalikuwa strong maneno serious watu 100 kufa sio kitu kidogo mpaka kutaja watu wa kabila fulani …ni sawa na kuwasha moto kwenye nyasi kavu…”
Hakimu Shaidi amesema kuwa jamii inawatu wenye uelewa tofauti kutokana na uwezo wa kuchuja maneno hivyo kila mmoja anaweza kuchuja maneni kwa kadri anavyoweza.
Baada ya kumtia hatia mshtakiwa Wakili wa Serikali Renatus Mkude ameitaka mahakam kumpa adhabu Zitto ilikuwa funzo kwa watu wengine.
Upande wa utetezi wakili Frank Mwakibolwa ameiomba mahakama hiyo kutotoa adhabu kali kwa kuwa mshtakiwa ni baba wa watoto wadogo wanne na kwamba hakuwa kuwa na rekodi za jinai kwenye mahakama.
Wakati huo huo Hakimu Shaidi alimpa adhabu ya kutoandika wala kutamka maneno ya uchochezi kwa muda wa mwaka mmoja.
“Ieleweke kuwa sisi sote Watanzania …tumlee mama yetu amani hata ninyi wanasiasa mnawajibu mkubwa wa kumtunza ”
“Mmezoe kusema kwenye mitandao kuwa Mahakama ya kisutu imegeuka TRA…”
Hakimu Shaidi amemaliza hukumu hiyo kwa kusema kuwa kama kuna upande haujaridhika na hukumu hiyo milango ya kukata rufaa ipo wazi.