Kama ulipitwa na habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania tayari millardayo.com imeshazikusanya na inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za hapa Tanzania leo April 25 2017.
Habari Clouds Tv: Wabadhirifu wasakwa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa saa 24 kuhakikisha kwamba watumishi 27 waliosababisha upotevu wa fedha na kulipana posho hewa za shilingi millioni 64 wanachukuliwa hatua mara moja wakiwemo wale waliohamishwa kituo cha kazi.
Habari Azam Two: Serikali yazungumzia hali ya Malaria nchini
Nchi tatu za Afrika zitafaidika na chanjo ya kwanza kabisa ya majaribio ya ugonjwa wa Malaria kwanzia mwakani na hiyo nikwamujibu wa shirika la afya duniani WHO, chanjo hiyo itajaribiwa kwakiwango kikubwa katika nchi za Ghana, Kenya na Malawi. wakati huo hapa nchini mawaziri wa wizara ya Afya wameelezea hali ya Malaria na jitihada zinazochukuliwa.
Habari Clouds Tv: Ajali ya barabani ya uwa watu zaidi ya 26 Kenya
Watu zaidi ya 26 wamefariki Dunia na wengine kujeruhiwa nchini Kenya baada ya ajali iliyotekea usiku wa kuamkia leo katika barabara ya kutokea Nairobi kwenda mjini Mombasa huku kamanda wa jeshi la polisi Leonard Kimaiyo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha basi la abilia na Lori
Chanel 10 Habari: Mahabusu wagomea kwenye karandinga
Mahabusu wagomea kushuka kwenye gari baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Arusha, huku wakidaiwa kuvua nguo ndani ya gari kwa madai yakutokutendewa haki na mahakama hiyo hivyo kusababisha taharuki na shughuli za mahakama kusimama kwa zaidi ya masaa mawili.
Chanel 10 Habari: Ufumbuzi wa malori yaliyokwama Zambia kupatikana ndani ya saa 72
Mawakili wa malori 600 yaliyokwama nchini Zambia wameahidiwa kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo ndani ya saa 72 kuanzia leo baada ya kufanyika kikao kizito baina ya ubalozi wa Zambia hapa nchini na wizara ya mambo ya nje.
VIDEO: Wizara ya katiba na sheria imeomba kutengewa zaidi ya Bilion 166