Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Mahakamani tena, kesi ya Zitto Kabwe yarudi… yakwama. (+video)

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kusikiliza ushahidi wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kwa sababu upande wa mashitaka umekosa kibali cha kuita Mashahidi kutoka Kigoma, hayo yamebainishwa na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Katika kesi hiyo ambayo ilipaswa kuendelea kwa Shahidi wa tano, Wakili Katuga amedai kuwa shauri hilo lilipangwa kusikilizwa na walishaanza utaratibu wa kupata Mashahidi kutokea Kigoma lakini wamekosa kibali kutoka kwa Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu.

Kutokana na hatua hiyo ya kukosa kibali, Wakili Katuga ameiomba Mahakama ifanye ahirisho wakati wakifatilia kibali hicho ili wawapate mashahidi hao ambao ni takribani sita kutokea Mkoani Kigoma, baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 16 na 17, 2019 ambapo Mbunge Zitto yupo nje kwa dhamana.

Katika kesi ya msingi, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi kwa kudaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 28, 2018 katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo, tazama hii video hapa chini Zitto Kabwe akiwa Mahakamani leo

EXCLUSIVE: NYUMBANI KWA BILIONEA MTANZANIA ALIEUZA JIWE LA ALMASI LENYE THAMANI YA BILIONI 3, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments