Top Stories

MAREKANI: Wazee 8 wamefariki kutokana na kukatika umeme

on

Wakati janga la kimbunga likiendelea kuleta maafa katika maeneo mbalimbali Marekani, wazee 8 wameripotiwa kufariki jana September 13, 2017 Florida kutokana na umeme kukatika katika eneo hilo na kuharibu huduma za afya.

Imeelezwa kuwa Kimbunga Irma ambacho kilipelekea kukatika kwa umeme katika kituo cha kuwatunza wazee kiitwacho ‘Hollywood Hills Rehabilitation Center’ kulifanya kituo hicho kubaki bila vifaa vya huduma za hewa ambavyo ndivyo vilitumika kushikilia uhai waa wazee hao walioishi kwa kujegemea kuwekewa hewa ya oxygen.

Mamlaka za usalama Florida kufuatia vifo vya watu hao 8 vimewahamisha wazee wengine 115 kutoka eneo hilo ambalo limefikwa na joto lililopindukia kutokana na kukatika kwa umeme. Watu takriban milioni 10 hawana umeme katika maeneo ya Florida, Georgia na Carolina.

Ulipitwa na hii? Paul Makonda anahamishia showroom zote Kigamboni

Hii je? WANAVYOISHI BUKOBA MWAKA MMOJA BAADA YA TETEMEKO

Soma na hizi

Tupia Comments