Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kuwa hadi sasa hivi haijapokea waraka wowote wa Kidplomasia kutoka nchini Marekani, unaoeleza kuwa Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zitawekewa vikwazo kwa raia wake kwenda nchini Marekani.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Emmanuel Buhohela, amesema kuwa hayo yanayoendelea ni maneno ya mitandaoni tu kutokana na kwamba wao hawajapata waraka wowote.
“Sisi kama Wizara mawasiliano yote huwa yanafanyika kwa Waraka maalumu wa Kidplomasia, ndio maana kuna Ubalozi kwahiyo kama kungekuwa na jambo lolote wangetueleza kwa kutumia njia hiyo, hadi sasa hatujapata ujumbe wowote na hatuwezi kuzungumzia vitu ambavyo vinasemwa kwenye mitandao” Buhohela.
WATANZANIA KUZUIWA KUINGIA MAREKANI, SABABU ZATAJWA (TRAVEL BAN)