Tangaza Hapa Ad

Michezo

Rekodi 10 za kufahamu kuelekea mechi ya kihistoria Man United vs Man City

on

Mashabiki wa soka ulimwenguni kote wanashauku ya kutaka kuona mchezo wa kwanza wa durby unaowakutanisha makocha wenye upinzania mkubwa Jose Mourinho na Pep Gurdiola, huu ni mchezo ambao unatajwa kuwa weekend hii utakusanya na kuangaliwa na mashabiki wengi, tayari magazeti ya England yameripoti maafisa usalama 400 kuwa watahudhuria mchezo huu.

Kuna vingi inawezekana ukawa hufahamu kuelekea mchezo huu unaotajwa kuwa ni wa kihistoria kutokana na upinzani wa vilabu vyenyewe na makocha husika

1- Vilabu vya Man United na Man City vimewahi kukutana mara 171, wakati Man United wameshinda jumla ya mechi 71 sare 51 na Man City wao wamefanikiwa kuifunga Man United mara 49, hivyo mchezo wa kesho utakuwa wa 172.

2- Kocha wa Man City Pep Guardiola na kocha wa Man United Jose Mourinho wamewahi kukutana mara 16 wakiwa wanafundisha vilabu vitano, wamewahi kukutana Mourinho akiwa na Real Madrid, Inter Milan na Chelsea wakati Pep alikuwa katika vilabu vya FC Barcelona na FC Bayern Munich hiyo ni katika kipindi cha miaka 7.

3-Pep Guardiola amemfunga mara nyingi zaidi Jose Mourinho, amewahi kumfunga mara 7 kati ya mechi 16, walizocheza, sare mechi 6 na Mourinho kamfunga Guardiola mara 3 pekee, Guardiola kamfunga Mourinho jumla ya goli 26 wakati Mourinho kamfunga Guardiola goli 16.

jose-mourinho-pep-guardiola-672846

4- Vilabu vya Man United na Man City katika michezo yao 171 waliyokutana wamefungana jumla ya magoli 484, wakati Man United wakiwa wameifunga Man City goli 250 na kuruhusu wao kufungwa magoli 234 tofauti ya goli 16.

5- Idadi magoli mengi aliwahi kufungwa Jose Mourinho na Pep Guardiola ni goli 5-0 ilikuwa November 9 2010 katika uwanja wa Nou Camp wakati Mourinho ushindi wake mnono aliyowahi kuupata kwa Pep Guardiola ni goli 3-1 akiwa Inter Milan April 20 2010.

6- Cristiano Ronaldo ndio mchezaji wa Man United aliyeoneshwa kadi nyekundu mara nyingi zaidi katika mchezo wa Man United dhidi ya Man City, ameoneshwa kadi nyekundu mara 2.

cr7

7- Man United ameshinda jumla ya mechi nne na sare 1 kati ya 5 za mwisho kabla ya kukutana na Man City kesho September 10, katika mechi 5 za Man City wao wameshinda jumla ya mechi zote 5.

8- Mara mwisho timu hizo kukutana katika mchezo wa Ligi Kuu England ilikuwa March 20 2016, mchezo ambao Man United walishinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Marcus Rashford dakika ya 16 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Juan Mata, ushindi ambao waliupata lakini Man City alitawala mchezo kwa asilimia 54 kwa 46.

MANCHESTER, ENGLAND - MARCH 20: Marcus Rashford of Manchester United celebrates as he scores their first goal during the Barclays Premier League match between Manchester City and Manchester United at Etihad Stadium on March 20, 2016 in Manchester, United Kingdom. (Photo by Michael Regan/Getty Images)

Marcus Rashford

9- Wayne Rooney ndio mchezaji anayeongoza kwa ufungaji magoli mengi katika durby ya Manchester, amefunga jumla ya goli 11.

sde

10- Jose Mourinho ametwaa jumla ya mataji 22 katika maisha yake ya ukocha, 8 ya Ligi Kuu wakati Pep Guardiola ametwaa mataji 6 ya Ligi Kuu lakini ana jumla ya mataji 21 amwzidiwa taji moja na Jose Mourinho.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement