Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya miezi kadhaa ya kukubaliana dili jipya, Neymar kafanya maamuzi

on

Ni miezi kadhaa imepita toka nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Brazil Neymar kutangazwa kufikia makubaliano na klabu yake ya FC Barcelona ya kuongeza mkataba, ila zoezi lilikuwa halijakamilika.

October 21 2016 klabu hiyo imetangaza kumsainisha Neymar mkataba mpya wa miaka mitatu, hivyo sasa ni rasmi Neymar ataendelea kuwepo Nou Camp hadi mwaka 2021 ndio mkataba wake utakuwa unamalizika.

neymar-signs-new-barcelona-contract-october-2016

Neymar mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na FC Barcelona mwaka 2013 akitokea klabu ya Santos ya kwao Brazil, kufutia mkataba huo Neymar katika msimu wa 2016/2017 atakuwa akilipwa mshahara wa euro milioni 18 kwa mwaka na msimu wa 2018 atalipwa euro milioni 25.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement