Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Na huyu ndio mrembo anaedai kuwa na ujauzito wa Davido

on

Screen Shot 2014-01-20 at 12.15.00 PMHii sio mara ya kwanza kusikia kajitokeza binti flani na kudai kazaa au ana ujauzito na staa flani wa muziki, movie, siasa au kingine chochote.

Sasa yule staa wa Nigeria ambae ndio yuko kwenye headlines na Diamond Platnums kutokana na kolabo yao ya ‘number 1 rmx’ yaani Davido, kimemkuta hiki cha huyu binti.

Mrembo huyu anaeishi Uingereza anaitwa Shanielle Sunshhine na amenukuliwa akisema wazi anao ujauzito wa Davido, ni ujauzito wa mapacha ulio na umri wa karibia miezi sita ambao ulitokana na kukutana kwao mwaka 2013 wakati Davido alipofanya Tour Uingereza.

Pamoja na kwamba Davido amekua kimya wakati wote kuhusu hii ishu, Shanielle amesema anakaribia kutoa vithibitisho vyote kwamba huo ujauzito ni wa Davido.

davido 1

davido 3

davido 23

Tupia Comments

Advertisement