Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Eti jeshi la Nigeria limewaambia nini Wasanii wanaovaa sare za jeshi kweye video?

on

NigeriaJeshi la Nigeria limetoa onyo kwa watu wote maarufu wa nchi hiyo kutovaa tena nguo za kijeshi uraiani na hata kwenye video zao kwa upande wa Wasanii kutokana na kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo.

Kwenye barua ya wazi iliyoandikwa na jeshi la nchi hiyo, kuna maneno yanasema ‘Ni marufuku kwa yeyote kuonekana na nguo za kijeshi popote, hii ni kwa Watu maarufu na wananchi wengine baada ya kugundulika pia nguo za kijeshi zimekua zikivaliwa kwenye music videos, photo shoots na kwenye matamasha’

Nigeria 2‘Vivyo hivyo, kwenye videos na photo sessions watu maarufu wa Nigeria kama Jesse Jags wameonekana wakivuta bangi wakati wako ndani ya mavazi ya kijeshi kitu ambacho ni kama kulichafua au kulidhalilisha jeshi, hivyo basi yeyote atakaepatikana na makosa haya hatua tutakazomchukulia hazitaulizwa au kuhojiwa’

Mastaa wengine wa Nigeria ambao hupenda kuvaa nguo za kijeshi ni pamoja na Iyanya, Wizkid, Davido, Tekno Miles, Chidinma.

nigeria 2nigeria 12

 

Tupia Comments

Advertisement