Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Farid Musa kuikosa Taifa Stars vs Benin kama Samatta

on

Ikiwa imepita siku moja tu toka jopo la madaktari club ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta, watoe taarifa kuwa Mbwana Samatta hatokuwa uwanjani hadi mwanzoni mwa kipindi cha majira ya baridi kufuatia kuumia kwa goti lake la kulia.

Leo taarifa mpya zimetolewa kuhusiana na mtanzania Farid Musa anayecheza soka la kulipwa nchini Hispania akiichezea Tenerife B, Farid Musa ambaye jina lake lilikuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza dhidi ya Benin November 12 2017, zimetoka taarifa kuwa ameumia goti.

Farid Musa anaripotiwa kuwa ameumia ligament za goti na anasubiri kufanyiwa vipimo vya mwisho ambayo vitatoa taarifa rasmi kuhusu muda atakaokaa nje staa huyo wa Tanzania lakini taarifa za awali zinaelewa kuwa kwa mujibu wa jeraha lake anaweza kukaa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia.

Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji

Soma na hizi

Tupia Comments