Habari za Mastaa

EXCLUSIVE:Miss Tanzania afunguka alivyotabiriwa na Mchungaji kushinda Miss World

on

Tunayo story kutokea kwa Miss Tanzania, QueenElizabeth Mkune ambapo amesema alishawahi kutabiriwa kushinda taji hilo la Miss Tanzania pamoja na Taji la Miss World, ambapo mashindano yake yanatarajiwa kufanyika Sanya, China December 8,2018.

Katika exclusive interview na Ayo Tv, QueenElizabeth amesema utabiri wa kushinda Miss Tanzania ulitolewa na Mchungaji wa kanisa la Ufunuo, Nabii Paul Bendera na kwamba sasa amemtabiria tena atashinda taji la Miss World.

“Siri ya mafanikio yangu ni Mungu, kwa sababu siwezi kushinda kwa sababu ni mrembo kwani wasichana wote ni warembo, hivyo kushinda kwangu ni kibali kutoka kwa Mungu.Pia kilichonishawishi ni kutaka kuwa Miss World,”amesema.

Pia QueenElizabeth amesema kabla ya kuwa Miss Tanzania alikuwa tayari ni mtu wa dini licha ya kuwa watu wanamwambia kwamba urembo hauingiliani na suala la kidini hasa kwa kuokoka.

VIDEO:Miss Tanzania alivyogusa ardhi ya Chuo anachosoma tangu ashinde Taji

Soma na hizi

Tupia Comments