Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Zari mbioni kufungua kliniki ya wanawake Dar?

on

Mwanadada Zari the boss lady ameingia tena kwenye headlines leo June 7,2018 baada ya kuwashangaza mashabiki kwa kuomba mchango wa dolla 1 ambayo ni shillingi 20,00 ya Kitanzania kwaajili ya kujenga kliniki ya wanawake DSM baada ya kufikisha mashabiki Milioni 4 katika mtandao wa instagram.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Zari ameandika “Wapendwa wangu Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema ASANTENI sana kwa 4M followers. ninyi ni ndugu kwangu, mmekua nami bega kwa bega kwenye shida na raha”

Sasa Mnichiangieni $1 kila mtu tujenge clinic ya wanawake sehemu yoyote dar, Najua tukiipata Baba Magufuli atatupa kiwanja….😁😁 #JustSayingPENDA SANA NYINYI.❤THANK YOU SO MUCH FOR 4M.
LOVE YOU ALL🌹”

Zari ametoa mawazo hayo na kusema kuwa endapo mashabiki hao millioni 4 watafanikiwa kufikisha kiwango flani cha fedha basi Rais JPM hatoshindwa kutoa kiwanja kwaajili ya kujenga kliniki hiyo itakayowasaidia wanawake lakini hajaweka wazi itakuwa inahusika na kutibu magonjwa gani zaidi.

Wimbo uliomfanya ‘Sam wa Ukweli’ ‘afie studio’ WALIMWENGU

Soma na hizi

Tupia Comments